MAMBO KAMA YALIVYO NJE YA TANZANIA

Friday, 9 September 2011

UNAIPATA HII ?

10:37 By Mindset




Kwa bongo ukiona hii unaweza kusema imekosewa kuandikwa TSHS. 250,85 ila kwa hapa Sauzi hii haijakosewa kabisa na inamaanisha ni Shilingi za kibongo 250 na senti 85. Nataka kusema nini hapa?, ni kuwa kwa Sauzi badala ya kutumia nukta kuonyesha desimali au senti mara nyingi hutumia alama ya ( ,) yaani koma.

Wakati bongo matumizi ya senti na shilingi moja ni kama yamesahaulika kwa sasa , si eti eeh ? nini wawezi nunua kwa shilingi mbili ? au nini waweza nunua kwa senti 75 ?
Hapa Sauzi bado fedha yao ina thamani kubwa na senti zinatumika kufanya malipo mengi tuu.

Mfano mfuko wa plastiki (Rambo) ni senti 35, wakati waweza nunua pipi kwa senti 20 mpaka 50 huku ukitakiwa kulipa malipo mengi mfano nauli ukitumia senti, mfano nauli ya sehemu A mpaka B yaweza kuwa Rand 4,50 ( yaani Rand 4 na Senti 50)

Si ajabu kukuta mtu akilipwa RAND ELFU MOJA MIA TANO kwa mwezi kama mshahara, wakati ukichota RAND 15000 kwa mwezi duh ! mambo yako safi sana !

John, Eastern Cape, SA.

0 comments: