MAMBO KAMA YALIVYO NJE YA TANZANIA

Friday 9 September 2011

PALE PAKA NA MBWA WANAPOPELEKWA HOSPITALI !

10:52 By Mindset


Ni jambo geni ufikapo hapa Sauzi au nchi nyingine zilizoendelea kukuta paka au mbwa akipelekwa hospital, tena hospitali maalum kwa ajili ya wanyama. Hili nimelishuhudia mwenyewe hapa Sauzi nilipokuwa Joberg, Cape Town na Durban, nilijionea kwa macho yangu hospital hizo na watu wakiwapeleka paka au mbwa kwa matibabu au kucheki tuu afya !!

Mdau wa marekani aishie Seattle, Washington amenidokeza hata huko hospitali za wanyama zipo na tena waweza mpeleka paka au mbwa akasafishwe meno !!.

Gharama ya kusafisha meno paka kwa eneo alilopo mdau wetu ni $ 250 sawa na kama TSHS. 408,750 za Kibongo.

Maendeleo bwana...!!

John, Eastern Cape , SA.

0 comments: