MAMBO KAMA YALIVYO NJE YA TANZANIA

Friday 9 September 2011

HILI NALO NENO !

10:01 By Mindset



Habari,
Leo niwajuze toka hapa Sauzi kuhusu malipo ya kila mwezi wanayopata makundi fulani ya watu.

Mfano, kila mama anayejifungua mtoto anao uwezo wa kudai toka serikalini fedha za malezi ya mtoto endapo hana uwezo wa kulea kichanga chake !

Wazee na walemavu pia hawajasaulika, endapo tuu wanaweza kuthibitisha kuwa kipato chao hakiwawezeshi kujikimu.

Sio tuu mafao hayo ila kuna mafao mengi ambayo wananchi au watu wenye kibali cha kudumu kukaa hapa Sauzi wanapata ili mradi wafuate masharti yaliyowekwa kama libeneke hili la serikali linavyoeleza:

http://www.services.gov.za/services/content/Home/ServicesForPeople/Socialbenefits/en_ZA

Kwa kifupi haya ndiyo ni baadhi ya mafao ya kila mwezi:

Mlemavu anajichotea kila mwezi Rand 1140 sawa na Tshs. 277,020

Mzee wa miaka chini ya 75, anakula Rand 1140 sawana Tshs. 277,020

Mzee wa miaka zaidi ya 75, anapiga Rand 1160 sawa na Tshs. 281,880

Wakati kila mafao kwa malezi ya mtoto ni Rand 260 sawa na Tshs.63 180

Upo Hapo !!
By John, Eastern Cape, SA.

0 comments: