MAMBO KAMA YALIVYO NJE YA TANZANIA

Wednesday 5 October 2011

TENNIS KWA WALEMAVU WA VIUNGO

09:21 By Mindset


Leo asubuhi nimejionea kwa taarifa ya habari mahojiano ya kituo cha TV cha etv na baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa ya Sauzi iliyoshiriki mashindano ya dunia ya Tennis kwa walemavu wa viungo maarufu kama WheelChair Tennis.
Nilichojifunza  ni kuwa kuna mashirika kadhaa dunia yanayotoa ufadhili kwa michezo ya walemavu na wanatoa msisitizo sana kushiriki. Naelewa pia kuwa kwa bongo tumewahi na labda bado michezo hiyo ya walemavu inaendelezwa. Kama unahitaji maelezo zaidi kuhusu mashirika hayo wasiliana na NJE YA BONGO.COM

Wenzetu Sauzi wamepiga hatua kubwa na mwaka kesho wanapeleka timu yao kwenye mashindano ya Olimpiki ya Walemavu. Pichani ni baadhi ya wachezaji wa Wheelchair tennis toka Sauzi.

( Picha na : themarketingsite.com , na gspot.co.za)
John.
Eastern Cape, Sauzi.

0 comments: