Kampuni ya Apple, jana ( Oktoba 4) imetangaza kutoa aina mpya ya simu ya mkononi inayoenda kwa jina la iPHONE 4S.
Tangazo hilo lilitolewa jana huko Marekani, wakati uzinduzi rasmi wa simu hiyo kwa nchi za Marekani, Canada, Australia, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Japani utafanyika Oktoba 14,2011 na kwa nchi nyingine zaidi ya 70 uzinduzi utafanyika ndani ya kipindi kilichobaki kabla ya kufunga mwaka 2011.
Simu hiyo ni 'kali' ikiwa na uwezo mkubwa wa sauti, kamera, uhifadhi wa taarifa, na zaidi sana waweza zungumza na simu hiyo, yenyewe ikafanya mambo yote. Mfano waweza kutamka meseji, na yenyewe ikaandika kisha ukaimbia itume na yenyewe ikatuma.
(Picha na apple.com)
1 comments:
Ni aina ya robot au?
Post a Comment