Mchungaji Skosana Xola (Pichani) kutoka kitongoji cha Khayelitsha ndani ya Cape Town amewaambia wafuasi wake kuwa Yesu alikuwa na HIV na kwamba hakuwabagua wagonja na aliwapenda watu wote kwa usawa.
Akitetea hoja yake, anasema lengo la fundisho lake si kumzalilisha Yesu bali kuibua hamasa na mwamko wa watu kufahamu ukimwi na kutowabagua wagonjwa na akaendelea kuongeza kuwa hakuna kipimo cha kisayansi kilichofanyika kuthibitisha kuwa Yesu alikuwa na UKIMWI au la.
Mchungaji Skosana Xola amepata umaarufu nchini hapa kwa fundisho lake hilo ingawa pia wengi wamempinga kwa kile walichokiita kumdhalilisha Yesu.
Mchungaji huyo ambaye amekuwa maarufu hivi karibuni ameibuka tena kwa runinga akiendesha kampeni ya kutokula ili kupinga huduma mbaya za serikali katika eneo lake.
Duh, Marketing strategies nyingine jamani !
Mdau, Sauzi.
2 comments:
Du! Huyu mchungaji kweli noma yaani hata haogopi kumzulia Muumba wetu!
Hii ya huyu mchungaji kali ,imenishangaza kwani yeye alijuaje? walimpima au imeandikwa katika kitabu gani kutoka kwenye Biblia? na ni dini gani kwanza? kwa hiyo yeye anamtangaza nani kama mchungaji?
Post a Comment