Swali hili tumeuliza kwa wadau wetu wa waliopo nje ya bongo ila ndani ya Afrika na jibu lilikuwa kwa wengi walisema ugali upo ila namna ya mapishi ni tofauti na bongo na majina yanatofautiana toka sehemu moja hadi sehemu nyingine.
Mfano, kwa Sauzi ugali unaitwa PAP, mapishi ni tofauti mara nyingi ni ugali mlaini, na wapo wanaochanganya mafuta na chumvi wakati wa mapishi na kitu kikiwa tayari basi mboga inaweza kuchanganywa juu ya ugali kama unavyoweza kuchanganya wali na mboga na ukatumia kijiko kwa kula.
La kutegemea pia ni kuwa hata radha ya vyakula yaweza kuwa tofauti kwani aina ya nafaka ni tofauti.
Hivyo kama wataka kupata msosi wa kibongo au fleva za kibongo, basi ujipikie au wakati mwingine wapo wabongo wanaofanya biashara ya kupika misosi kama hiyo ya kibongo.
0 comments:
Post a Comment