MAMBO KAMA YALIVYO NJE YA TANZANIA

Monday 19 September 2011

KAMPENI YA KITAIFA DHIDI YA 'KILAJI'

14:10 By Mindset



Baada ya kuona hali si nzuri kutokana na utumiaji wa hali ya juu wa kilevi, serikali ya Sauzi ilitumia siku 5 (Septemba 5 mpaka 9 mwaka huu) kufanya kampeni rasmi kuhusu kilevi, ikielimisha wananchi madhara ya utumiaji wa pombe kwa kupindukia na pia kuelemisha kuhusu utoaji wa leseni za kufungua baa ( hapa zinaitwa TAVERN) pamoja na vituo vingine vya uuzaji wa kilevi.

Inasemwa hapa kuwa 'kilaji' ni chanzo namba tatu cha vifo vingi vya watu, huku ikiingiza hasara serikali ya kadirio la Rand bilioni 9.

Hata hivyo inasemwa kuwa 'kilaji' kinaliingizia taifa wastani wa Randi bilioni 94.2.

Kwa maelezo zaidi kuhusu kampeni hii bofya hapa

0 comments: