Salam,
Hii ni orodha ya gharama za kawaida na za kila siku endapo unafikiria kutembelea Sauzi, na kama unawaza kuishi maisha ya kawaida. Ila kama unatarajia ku 'spend' kama mtalii, basi zidisha hapo kama mara tatu hivi...
Msosi (Mlo mmoja) Rand 30-50 sawa na Tshs.7,290 hadi Tshs. 12,150
Guest ( B &B) ni Rand 250 kwa mtu mmoja, hivyo kama upo na partner ni R500 sawa na Tshs.60,750 kwa mtu mmoja au Tshs.121,500 kwa usiku mmoja.
Usafiri wa daladala (ambapo hapa zinaitwa TAXI) ni kati ya R5 -12 toka sehemu A kwenda B, ni kama Tshs.1,215 - Tshs.2916
Kama unafikiria kukodi Taxi, hapa Taxi zinachaji kwa umbali (zina mita ndio maana zinaitwa Meter Taxi) hivyo si rahisi kukutajia gharama ila umbali mdogo zaidi waweza lipa Rand 30 sawa na Tshs.7,290.
Kama unafikiria kukaa muda mrefu hivyo labda upange chumba, basi kodi ni kuanzia Randi 1,000 sawa na Tshs.243,000 kwa mwezi, na uzuri wa Sauzi sio lazima ulipe kwa mkupuo, waweza kuwa unalipa kila mwezi, hakuna cha miezi sita au cha mwaka.
Umeme kama umepanga yaweza fika kama Randi 300 sawa na Tshs.72,900
Wakati maji yaweza kuwa ni Randi 200 sawa na Tshs. 48,600.
Usafiri wa Mikoani kwa basi ni kati ya R 250 hadi 600 kutegemeana na eneo, hii ni Tshs. 60,750 hadi Tshs.145,800
Upo Hapo...!
By John, Eastern Cape, SA.
0 comments:
Post a Comment