Ndugu John,
Nakusalimu wewe na wadau wengine wa blogu hii.
Nakushukuru kwa wazo zuri la kuwa na blogu hii na ninapenda kueleleza dukuduku langu kama ifuatavyo
Blogu hii kwa ninavyoiona inatupa nafasi watanzania popote pale tulipo nafasi ya kujifunza mambo ya nchi nyingine na hasa ya msingi ili hata tukitembelea huko tuwe na taarifa za awali kabla ya kutembelea maeneo husika.
Dunia hii ya utandawazi inatuweka katika nafasi ya kuwa wasafiri sio tuu kwenda kuishi nje ya nchi lakini inatupa nafasi ya kutembea nchi nyingine kwa sababu mbalimbali kama vile Masomoni, Ziara za kikazi, matibabu na hata mapumziko. Hivyo naona wazo la hii blogu litawasaidia watu wengi sana.
Naomba wale wote wenye taarifa muhimu kwa blogu hii tuendelee kujuzana kwani jambo hili la kushare taarifa sio geni, mbona tunafanya hivyo kupitia facebook na mitandao mingine hata kupitia email. Naomba tulipe jambo hili uzito wa namna yake kwani ni jambo la msingi sana kwani kwa namna moja au nyingine sote ni wasafiri watarajiwa wa nje ya Tanzania iwe kwenda kimatibabu, ziara ya kikazi, masomoni au matembezi tuu.
Na mwisho naomba unijuze taarifa za gharama za maisha za kawaida kwa nchi ya Malaysia, kwani natarajia kuenda kusoma huko mwakani, mungu akipenda. Nilipenda sana ile taarifa za gharama kama hizo kwa nchi ya Afrika Kusini.
Ahsante,
Mdau, Dar es salaam.Tanzania.
N:B Tunashukuru sana mdau wetu wa Dar es salaam (umeomba tusitaje jina lako) kwa email yako. Tuendelee kuwa pamoja, ni kweli ni kwa ushirikiano tuu blogu hii itafikia lengo lake la kujuzana.
Wadau kama mlivyosikia mdau wetu wa Dar es salaam anaomba yeyote anayejua gharama za maisha kama misosi, pango la nyumba, umeme, nauli za mabasi, nguo, hoteli, n.k kwa nchi ya MALAYSIA tujuzane.
Kama una taarifa, tuma kwa email yetu hapo juu, nasi tutaziweka hewani. Shukrani.
NJE YA BONGO.COM
0 comments:
Post a Comment