MAMBO KAMA YALIVYO NJE YA TANZANIA

Wednesday 21 September 2011

OMBI LA TAARIFA ZA VYUO NJE YA BONGO

15:33 By Mindset

Tumepokea maombi ya taarifa kuhusu vyuo nchini Afrika Kusini, kuhusu taarifa za ada,  vibali vya kuishi, kodi,  gharama za makazi, na wastani wa bajeti ya maisha kwa ujumla. Wadau wawili wameuliza hili wakitaja lengo lao la kufika Sauzi kufanya Masters Degree.


Pia mdau mmoja anaomba kujua taarifa za aina za magari toka Afrika kusini na gharama zake. Na anaomba utofauti wa magari ya Japani na Sauzi.

Yeyote mwenye kuweza kuchangia hoja hii na pia mwenye taarifa kama hizo kwa nchi nyingine tafadhali wasiliana nasi kwa: john.myungire@gmail.com

Kwa wadau walioomba taarifa hizo, tunaziandaa, na tutazipost kesho mchana kwa saa za Afrika Mashariki.

Ahsanteni, Tupo Pamoja.

NJE  YA BONGO.COM

0 comments: