MAMBO KAMA YALIVYO NJE YA TANZANIA

Thursday, 15 September 2011

BABA WA TAIFA ANAVYOENZIWA NJE YA BONGO

14:36 By John MyungireHivi ndivyo wenzetu wa Sauzi wanavyomuenzi Mzee Nelson Mandela ambaye kwao ni kama alivyo hayati mzee wetu J.K Nyerere kwa Tanzania.

Hii ni taswira ya jengo kubwa lililojaa taarifa za historia ya maisha ya mzee Mandela toka akiwa mdogo, akiwa shule, pilika pilika za uhuru, na hata alivyokuwa jela.

Inapendeza ukiingia ndani jinsi ilivyopangiliwa, achilia mbali fursa ya kuisikiliza na kuona kwa runinga hotuba zake mzee huyu aliyejizolea heshima kubwa ndani na nje ya bara la Afrika.

Hapa ni Mthatha, jimbo la Eastern Cape.

Mdau, SA.

0 comments: