Anaitwa Kang Mengru, kutoka jiji la Luohe jimbo la Zhenzhou aligundulika kuwa na uvimbe tumboni ambapo majirani walianza kunong'ona kuwa eti alikuwa 'mjauzito'.
Mtoto Kang alitelekezwa na wazazi wake muda mfupi baada ya kuzaliwa hivyo akaishia kuchukuliwa na wanandoa wawili ambao hawakubahatika kuwa na mtoto.
Madaktari baada ya uchunguzi waligundua kuwa tatizo alilokuwa nalo Kang, linaelezeka kisayansi kuwa kuna wakati watoto mapacha huzaliwa na ikatokea mmoja kuwa na uvimbe unaofanana na kiumbe hai ndani ya mwenzake - kisayansi inaitwa Fetus in Fetu.
Baada ya operesheni ya masaa 10, 'kitoto' kilichokuwa ndani ya mtoto Kang kilitolewa na Kang aliendelea kuwa mzima.
Matukio mengine yanayofanana na Kang - yaani mtoto kuwa ndani ya mtoto mwingine yanatajwa kama ifuatavyo kwa wikipedia.com
Septemba 2011 Mwanaume wa miaka 41 wa huko Indonesia aligundulika kuwa na 'mimba' ambapo uchunguzi ulionyesha uvimbe unaojulikana kama Fetus.
Mwaka 2003 kijana Alamjan Nematilaev wa umri wa miaka 7 alifanyiwa upasuaji ili kuondoa fetus, kiumbe ambacho kilikuwa kikikua ndani ya mwili wake.
Mwaka 1999, Sanju Bhagat wa huko Nagpur India akiwa na umri wa miaka 36 naye aligundulika kuwa na kiumbe tumboni mwake ambacho kilikua sana.
Kwa Matukio mengine zaidi ya Fetus in Fetu BOFYA HAPA
Matukio ya kuwepo Kiumbe ndani ya kiumbe mwingine yaani Fetus in Fetu ni nadra sana, wataalamu wanasema hutokea mara 1 kwa kila watoto wachanga 500,000 wanaozaliwa hai.

0 comments:
Post a Comment