Anaitwa Pablo Emilio Escobar aliyezaliwa mwaka 1949, na kufariki mwaka 1993 wakati wa mapambano makali na askari wa jeshi la Colombia wakisaidiwa na Marekani.
Escobar alikacha shule, na kujihusisha na utapeli, wizi na hatimaye biashara iliyompatia utajiri na umaarufu mkubwa,biashara ya madawa ya kulevya.
Escobar alimiliki majengo ya kifahari, magari ya kifahari na hata ndege. Aliwahi pia kushika nyazifa ya kisiasa.
Escobar alikuwa akitafutwa na askari wa Marekani na Colombia kwani biashara yake kubwa iliharibu maisha ya watu wengi huko Colombia na Marekani. Alikuwa ni mtu aliyelindwa na katili sana, kuwa wakati alinukuliwa akijifananisha na Mungu akisema: Kuna nyakati Mimi ni Kama Mungu, kama nikisema mtu afe basi siku hiyo hiyo anakufa.
Ingawa dau la dola za kimarekani Milioni 20 kwa yeyote ambaye angefanikisha kupatikana kwake, hakuna mtu aliyethubutu kutaja alipo ingawa inadaiwa wananchi wengi wa mji alipokuwa akiishi wa Medellin huko Colombia walijua nyendo zake.
Biashara ya Escobar ilikuwa juu ambapo katika kwa mwezi walikuwa wakitumia takribani Milioni 4 , shilingi za kitanzania kununulia raba bendi za kufungia maburungutu ya hela ambazo kwa kuwa zilikuwa fedha haramu hawakuweza kuziweka benki badala yake waliziweka kwa maghala yao ambapo kila mwaka walipoteza 10% ya fedha hizo kwa uchakavu.
Escobar aliuawa karibu katika nyumba iliyokuwa karibu na kiwanja vikubwa vya mpira hapa Medellin , Colombia, wenyeji wanasema siku aliyouawa ilikuwa ni siku ya mechi kubwa ya soka lakini kwa umaarufu wake mashabiki waliacha kuangalia soka wakaenda kuangalia mwili wa Escobar.
Maelezo haya kwa hisani ya wikipedia na mdau wetu aliyepo Colombia
0 comments:
Post a Comment