Jumatano tarehe 12/10/2011 Mwalimu mmoja wa kike wa umri wa miaka 44 ambaye jina lake halikutajwa aliamua kujichoma moto huko Ufaransa akidai anafanya hivyo kwa kuwa wanafunzi wake ni vibuli - hawasikii na wanapiga sana kelele darasani.
Mwalimu huyo wa Hesabu katika shule ya sekondari ya Beziers, alifanya tukio hilo mbele ya wanafunzi wake tena kweupe kwenye uwanja wa michezo wa shule hiyo. Kwanza alichukua kimiminika kinachosadikiwa kuwa ni Petrol akajimwagia, kisha akajiwasha kwa kiwasha moto.
Kuonyesha kuwa alidhamiria kujichoma, hata walimu wenzake na watu wengine walipojitokeza kumsaidia alionyesha ukaidi wa kutotaka msaada akidai eti Mungu kamuagiza ajichome.
Hata hivyo wadau mbalimbali wa shule hiyo walifanikiwa kumuokoa mwalimu huyo na kumuwahishha hospitali ambako pamoja na juhudi za madaktari maalum wa majeraha ya moto, Mwalimu huyo aliaga dunia siku ya Ijumaa tarehe 14/10/2011.
Tukio la mwalimu huyo limezua mjadala huko Beziers, Ufaransa kuwa inabidi mamlaka husika ziangalie upya mazingira ya kazi ya walimu kwani aliyoyafanya mwalimu huyo ni kielelezo tosha cha ugumu wa mazingira wanayokumbana nayo walimu.
Taarifa kwa mujibu wa Yahoo contribution network na google.
COMMENT yetu NJE YA BONGO.COM : Kumbe ugumu wa mazingira ya kazi ya walimu sio tuu Tanzania !!
4 comments:
Sio bureee Hiyo ni bange kabisa!!! Kelele za wanafunzi na kujiua wapi na wapi? Hii ya kujifunzia ukubwani inashida yake!
Sio bureee Hiyo ni bange kabisa!!! Kelele za wanafunzi na kujiua wapi na wapi? Hii ya kujifunzia ukubwani inashida yake!
teh teh teh teh duuuh hata nashindwa nicoments nini mana si mchezo......
Sasa Mwl kama huyu angeletwa shule za bongo especially za kata zenye watoto watukutu kibao na vifaa vya kufundishia havitoshi madarasa yana vumbi walimu hawatoshi naona angejinyonga huku anajichoma moto!
Post a Comment