MAMBO KAMA YALIVYO NJE YA TANZANIA

Thursday 29 December 2011

RIPOTI KUTOKA COLOMBIA

18:52 By Mindset

Kuna watu weusi wengi tuu, na watu wenye mchanganyiko wa rangi - Africast ni wengi.
Wapo watu wa dini mbalimbali. Kuna uhuru na kuheshimiana sana katika maamuzi ya kuabudu. Mfano mzuri ni familia niliyofikia hapa Medellin, Colombia kuna mdada mmoja , wa miaka 20 hivi, wote katika familia yake ni wakristu ila yeye ameamua kuwa muislamu na anavaa hata hijabu. Hajaolewa bado na hakuna ushahidi wa haraka kama ana mchumba wa kiislamu. Familia yake ingawa haielewi kwanini kabadili dini, wameamua kuheshimu maamuzi yake na wanashirikiana naye katika yote.

Katika maswala ya kibiashara, wenzetu wanapenda sana kufahamiana na mtu husika vyema kabla hawajafanya biashara. Hapa mkutano wa kibiashara (Business meeting/lunch) yaweza kuchukua hata masaa manne, ambapo huzungumza mambo ya kijamii na kufahamiana, ambapo mwishoni waweza kutaja mambo ya kimsingi ya kibiashara na kuacha mkataba mtu akaufikirie.

Sehemu nyingi kazi huanza saa tatu asubuhi, muda wa mapumziko ya lunch ni kati ya masaa mawili hadi matatu, halafu shughuli huendelea hadi saa moja usiku.

Sehemu kubwa ya maisha ya watu wa hapa ni katika familia ambapo mtu hukua na kuishi na familia

yake hata akiwa na umri mkubwa. Hii ni tofauti na nyingi hasa za Ulaya na Amerika ya Kaskazini.

Midundo maarufu ya ngoma hapa ni Charanga maarufu kama SALSA. Pata jionee charanga hapa chini linavyosakatwa.
Mdau,
Medellin, Colombia

0 comments: