MAMBO KAMA YALIVYO NJE YA TANZANIA

Monday, 12 December 2011

OFA KWA BIASHARA NDOGO NA ZA KATI TOKA GOOGLE

03:54 By Mindset

NEW DELHI: Wafanyabiashara wadogo na wakati nchini India watapatiwa huduma ya kuwa na website zao bure kutoka kwa kampuni kubwa ya mawasiliano ya Google.
Kwa mujibu wa Times of India Google itatoa huduma ya kiwango cha juu kabisa kwa makampuni yatakayojiandikisha kwa mpango huo maalum unaoitwa “India Get Your Business Online”. Website zitakazotengenezwa zitawekwa hewani bure na kampuni ya kimarekani ya HostGator.
Biashara zitakazojiandikisha kwa mpango huu zitaweza pia kupata anuani za barua pepe za bure , na huduma ya kutangaza biashara zao na Google ijulikanayo kama Google AdWords yenye thamani ya dola za kimarekani 51 (sawa na takribani shilingi za kitanzania 85,000).
India ni nchi ya 18 katika mpango huo wa huduma za bure toka Google, mpango ambao ulianza mwaka 2010 mahsusi kwa nchi za Ulaya.
Wakati inakadiriwa jumla ya biashara za ndogo na za kati (SME) nchini India ni milioni 8, kwa mujibu wa takwimu za Google, 5% tuu ya hizo biashara ndizo zenye website.
HIVI OFA HII INGEKUJA BONGO INGEKUWAJE? TOA MAONI YAKO.

0 comments: