MAMBO KAMA YALIVYO NJE YA TANZANIA

Tuesday 8 November 2011

DANSI LA BABA NA BINTI - UTAMADUNI WA KIMAGHARIBI

12:28 By Mindset


Sherehe nyingi za harusi katika nchi za magharibi hapa namaanisha Ulaya na Amerika, huwa na kibwagizo katika ratiba zake ambapo baba wa bibi harusi hutakiwa kufungua muziki na binti yake.

Ingawa si sherehe zote huwa na dansi hili, ila nyingi zinazokuwa na dansi hili huvutia sana. Endapo baba wa bibi harusi hayupo basi mtu yeyote wa makamo toka upande wa bibi harusi kama vile mjomba, au baba mkubwa, huingiza stejini kusakata muziki na bibi harusi.

Jionee, kwa video hiyo moja ya dansi la Baba na Binti - huko Marekani. Dansi hii ilifunika. Angalia mpaka mwisho.

1 comments:

furaha said...

teh teh teh teh ipo njema ila baba hapo baba yako inabidi ajitoe ufahamu kama hyo