Kama una mpango ya kufanya kazi ya maana ‘decent job’ nje ya Tanzania, basi tambua yafuatayo ambayo wengi waliopo nje ya bongo wakifanya kazi za maana kama wahasibu, wahandisi, madaktari, waalimu na wahadhiri niliozungumza nao wametaja kuwa ni ya msingi kuzingatia:-
1. 1.Tambua fani yako ni ipi (profession) na uwe bora katika hiyo. Namaanisha uwe kweli na uelewa na uwezo wa kuleta utofauti wa uzalishaji kupitia fani yako. Kwani wetu imekuwa ni kasumba kuwa na elimu ya darasani tuu –yaani kuwa na vyeti ila hatuna uwezo hasa wa kuchanganua mambo na kufanya uzalishaji wa utofauti katika fani tulizopo. Jiulize wewe katika hiyo fani yako, mfano ni mhasibu, mhandisi, geologist, au IT specialist je upo hasa Competent katika nini hasa ?
2. 2. Uzoefu ni muhimu sana ili uweze kweli kuonyesha utofauti kati yako na watu wengine waliopo nje ya Tanzania. Kumbuka hata huko nje ya nchi unakotaka kuenda kuna watu wenye profession yako na kila nchi ina tatizo la ukosefu wa ajira na sheria ni ngumu
3. 3. Kujiamini: Hili linategemea sana mambo mawili hapo juu yaani kujitambua upo mzuri katika nini kwa fani yako na uzoefu ulionao katika hilo. Ukijiamini unaweza kuaply kwa ujasiri kupitia mitandao kibao kama unavyoweza kusearch kwa google. Tumeandaa orodha ya asasi zinazoweza kukusaidia kupata ajira nje ya Tanzania, tutaziweka hewani hivi karibu. Endelea kutembelea blogu hii.
Mambo mengine yanaweza kusaidia sana kushindana katika soko la kimataifa la ajira ni pamoja na:
1. 1. Teknolojia: Uwezo wa juu katika matumizi ya teknolojia hasa software mbalimbali ni jambo linaloweza kukuweka uwe tofauti na wengine. Hapa nazungumzia software muhimu. Mdau wetu ambaye ni Mhandisi ambaye ndani ya mwaka mmoja ameshafanya kazi na makampuni tofauti tofauti nje ya bongo, anasisitiza kuwa uelewa mkubwa wa software zinaendana na kazi husika unasaidia
2. 2. Lugha: Wengi wetu hata baada ya kumaliza digrii bado english ni tatizo. Hili haliwezi saidia kwani unahitaji sana lugha kujielezea, kuandaa ripoti, na kuonyesha kujiamini katika uwezo ulionao kufanya kazi. Ujuzi wa lugha zaidi ya English ni muhimu, ingawa kama unapenda kujifunza, haitakuwa ngumu kujifunza lugha nyingine mara utakapohitajika kufanya hivyo . Ila kwa kuanzia na kama unamuda sio mbaya ukajua Spanish, French, kijerumani, Kiitaliano na Kireno.
Yote kwa yote kumbuka kuwa kufanya kazi nje ya nchi kwanza utahitaji VISA ya kuingia nchi husika, kisha kibali cha kufanya kazi. Kuvipata hivi vyote huchukua muda na wakati mwingine ni gharama sana, nap engine usipate. Ila kama una sifa za kipekee za kupata kazi nje ya bongo, basi kampuni au shirika husika linalokuhitaji litashughulikia hayo yote na hapo utauona urahisi wa mambo.
N:B Maelezo haya hayana lengo la kuwa ushauri binafsi kwa yeyote anayetaka kupata kazi nje ya Tanzania, bali ni mtazamo tuu wetu na wengi tulioongea nao ambao wapo nje ya Tanzania wakifanya kazi.
0 comments:
Post a Comment