MAMBO KAMA YALIVYO NJE YA TANZANIA

Thursday, 6 October 2011

SHERIA HII INGEKUWA KATIKA SOKA !!!

10:10 By Mindset

Rugby ni mchezo unaoshangaza sana kama ni mara yako ya kwanza kuona wakicheza. Kuna mambo mengi sana tofauti na soka ingawa wapo wanaouita mchezo huo 'footbal'.

Ingawaje miguu hutumika pia kucheza mchezo huu, ila muda mwingi mikono hutumika. Idadi ya wachezaji wa kila timu ni KUMI NA TANO UWANJANI, hivyo jumla ya wachezaji uwanjani ni THELATHINI.

Ingawa kuna magoli kama vile ilivyo soka, magoli haya ni marefu sana, yana umbo la H na hayana golikipa. Cha kushangaza zaidi ni kuwa refa anaruhusiwa kusimamisha mchezo kama goli limeingia na kuna ulalamishi wa kama ni goli au laa. Sheria hii inaitwa TMO ( Television Match Official) ambapo refa husubiri maamuzi toka nje kwa maofisa maalum wanaoangalia mchezo katika runinga. Kama unavyojionea pichani, ni mojawapo ya mechi za Rugby ambapo Refa anasikiliza maelekezo toka nje ya uwanja.

Lingine kwa upande wa uamuzi, kuna marefa watatu, ambapo refa mkuu huwa kati, lakini waliopo nje wanamsaidia pia kucheki faulo na mwenendo mzima wa mchezo.

Mabingwa wa Rugby duniani kwa sasa ni SAUZI.

(Picha na: news.bbc.co.uk/)

0 comments: