Wanajimu na wafuatiliaji wa kalenda ya Mesoamerican Long Count wanadai kuwa mwezi Desemba mwakani utakuwa ni mwezi ambao dunia na vyote vilivyomo vitabadilika kwani huo utakuwa ndio mwisho wa zama hizi za kuishi, na vyote vilivyomo vitakuja kuwa katika mfumo mwingine, ingawa hawataji itakuwaje ila msisitizo ni kuwa itakuwa ni mwisho wa dunia.
Kuna website maalum kwa maelezo haya ya mwisho wa dunia 2012, bofya hapa endworld2012.com
Hata hivyo wataalamu wa kada mbalimbali wametupilia mbali 'uzushi' huo wa mwisho wa dunia. Ikumbukwe pia bado tupo katika kipindi ambacho Mchungaji wa Kimarekani - Harold Camping amedai Oktoba 21, mwaka huu ndio mwisho wa dunia.
2 comments:
Ngoja tusubirie maana hatuna jinsi
mmmmh nshachoka kusikia hzo habari mana tangu nazaliwa nasikia mwisho wa dunia, hata haufiki mwisho wa dunia ni kufa kwako. thus all!!!!
Post a Comment