MAMBO KAMA YALIVYO NJE YA TANZANIA

Thursday, 29 September 2011

BABU ALIYEDAI MWISHO WA DUNIA MAY 21 HUYU HAPA

14:37 By Mindset



Mbabu wa miaka 90, Harold Camping  (pichani) aliwapagaisha baadhi ya watu alipodai kuwa mwisho wa dunia ni May 21, 2011. Mzee huyo anayeishi California, Marekani, alitumia vifungu kadhaa vya biblia kusisitiza kuwa piga ua May 21 dunia itaanza kuteketea taratibu kabla ya ule mwisho wenyewe ambao alitaja utakuwa tarehe 21 Oktoba, 2011.

Hata hivyo mzee huyo ilipofika May 21,2011 aliingia mitini hakusema kitu mpaka siku kadhaa zilipita kisha akatoa tamko lake akielezea kuwa alikosea 'Mahesabu' na sasa amepitia vyema 'mahesabu' yake na kuwa Oktoba 21,2011 ndiyo mwisho kabisa akidai Mungu hajapenda kuona watu wakiangamia kwa muda mrefu toka May 21,2011 hadi Oktoba 2011, bali ameifanya siku ya mwisho wa dunia kuwa moja tuu yaani Oktoba 21,2011.

Mamia ya watu waliamini hilo na kuna waliouza mali zao na kuziwasilisha kwa kanisa lake huku wakisahau kuwa mzee huyo huyo aliwahi kutabiri mwisho wa dunia ungekuwa Septemba7, 1994 na kabla ya hapo aliwahi kudai mwisho wa dunia ungekuwa May 21, 1988.

Mzee huyo ambaye alianza kazi ya uchungaji mwaka 1958, anamiliki kituo kikubwa cha radio cha habari za kidini. Kitaaluma mchungaji Harold Camping ni Mhandisi (Civil Engineer) aliyegraduu katika chuo cha California University, Barkeley mwaka 1942.

(Maelezo kwa hisani ya wikipedia, Picha na: National Geographic.com)

1 comments:

Herman Makundi said...

anazeeka vibaya kwa kweli