Kutoka London, Uingereza
Asikwambie mtu, ukipata nafasi ya kufika uwanjani kucheki mechi ya Champions League, ni burudani ya kipekee.
Kilichonigusa zaidi, ni kusikia ule wimbo maarufu wa UEFA Champions league ukipigwa wakati wachezaji wamejipanga uwanjani.
Kwa kawaida wimbo huu tunausikia kipande kidogo tuu, kwa TV wakati wa mechi za UEFA Champions League.
Ikanivuta kuutafuta online kupata maneno yake kwani nilipousikia vizuri uwanjani ni kama mchanganyiko wa lugha kadhaa.
Ni kweli, wimbo huo umeimbwa katika lugha kuu tatu French, English na Germany.
Ulitungwa na Muingereza Tony Britten mwaka 1992.
Mdau, UK.
0 comments:
Post a Comment