MAMBO KAMA YALIVYO NJE YA TANZANIA

Saturday 24 September 2011

UBUNIFU

10:50 By Mindset

Ili kusimamisha gari likupeleke sehemu husika, wakati fulani inabidi uwe na bango kama hilo pichani kuonyesha wapi unaenda. Mara nyingi hapa Sauzi watu hutumia vifupi maalum vya mahali husika, mfano PE inamaanisha Port Elizabeth.


Kuna sehemu maalum za kusimamisha magari maarufu kama Hiking Spot, au wakati mwingine watu husubiria magari sehemu za mataa huku wakiwa na mabango/karatasi iliyoandikwa kifupi cha mahali wanapoenda.

Hii inarahisisha mawasiliano na madereva wa magari binafsi ambao kama hawaendi sehemu husika iliyoandikwa katika karatasi , waendelee na safari.

Walengwa wakubwa wa Hiking spot ni magari binafsi ambayo hayafanyi biashara ya kusafirisha abiria bali yapo safarini kuenda sehemu husika. Malipo ya safari mara nyingi yanajulika.

John, Sauzi.

1 comments:

Mbega said...

That is nice .. Bongo kungekuwa na kitu kama hiko safi sana. Sometimes unakuta mtu yupo peke yake na angependa kupata abiria but akifikiria kwenda kutafuta madalali stend anaona aah bora tu aghairishe.