MAMBO KAMA YALIVYO NJE YA TANZANIA

Tuesday, 27 September 2011

ORIJINO ALADJI TOKA IVORY COAST

09:49 By Mindset


Wimbo huu wa Aladji, umepata umaarufu sana bongo.

Mdundo huo wa ngoma ni maarufu nchini Ivory Coast, mtindo huo wa muziki unaenda kwa jina la Coupé-Décalé. Mtindo huu wa uchezaji ni maarufu pia katika nchi kadhaa za Afrika Magharibi.


Kwa tafsiri ya harakaharaka aladji maana yake ni mtu wa nyazifa fulani hasa ya kifedha - mtu mzito, jina ambalo hutumika pia kumaanisha mtu muislam. Wenye kuifahamu nyimbo vizuri maeneo ya hapa wanadai jamaa aliimba hiyo nyimbo mahsusi kwa hao aladji kuwa wanaweza pia kucheza hiyo nyimbo - aladji mara nyingi huvaa nguo kubwa kubwa kama unavyoweza ona hapo kwa video.


Hii inatupa sura nyingine ya maisha nje ya bongo. Embu fikiria hiyo ndiyo kama bongo fleva yetu. 


We bana !


Mdau, Cameroon.



0 comments: