MAMBO KAMA YALIVYO NJE YA TANZANIA

Monday 19 September 2011

MTAZAMO MWINGINE WA NJE YA BONGO

10:12 By Mindset




         Hizi picha sikupiga kijijini, hapana ni mjini. Nyumba hizi maarufu kama 'shacks' hapa Sauzi.

Kitu nilichojifunza nikiwa nje ya TZ ni kuwa unapokuwa bongo unakuwa na mtazamo wa juu sana kuhusu nchi zilizoendelea kama Sauzi.

Ila unapofika nchi husika, maisha yanakuwa tofauti na unatambua mambo mengine tofauti kabisa, mfano wengi ukiwaambia hiyo picha ni Sauzi hawawezi amini. Ila wapo wabongo ambao wanaishi kwenye nyumba kama hizo hapa Sauzi.


Yes, zipo sehemu zilizoendelea sana na sehemu zilichochoka vibaya  hata ndani ya Joberg, na Cape Town.

Mdau toka USA, anaongeza kuwa hata huko USA wapo watu wanaishi maisha ya chini sana, na hata kuomba omba mitaani.

Hapa Sauzi, kwa baadhi ya miji ni jambo la kawaida kumkuta mtu mweupe (Mzungu) dereva wa basi la abiria, mhudumu katika kituo cha mafuta, au muongoza magari katika sehemu za kupaki magari hata katika Shopping Malls.

Ila Yote Maisha.....!
By John, Sauzi.

0 comments: