Kutembea ni heri kuliko kukaa sehemu moja,nafarijika sana kwa umri nilio nao kusafiri mabara matatu yah ii dunia yetu,ASIA,EUROPE,AMERICA,nimejifunza mengi sana katika safari zangu zote nilizofanya,nimepata kujua mengi sana na kuona tulivyo nyuma kimaisha na kifikra na hatujui,na tunavyochezea muda na wakati katika maisha na afya zetu pia,pia serikali yetu inavyochezea maliasili tulizo nazo.
Nimejifunza utamaduni tofauti na kujua baadhi ya lugha tofauti,Arabic,Spanish,Italian,Indian,English,tuna kazi ndefu sana ya kuijenga nchi yetu na bara letu la Africa,
Niliyo jifunza Dubai:
Mpangilio wa mji wao na kila kitu,kwanza Dubai international airport,ni airport nzuri ya kisasa sana dunian inasemekana ndio airport ya kifahari sana dunian...mwanzoni niliwaza airport maarufu ya Amsterdam ya Schiphol ndio ya kisasa zaidi,kumbe siyo ndio maana nasema tutembee tujue mengi..nilifika Amsterdam mwaka 2011,November 25,na shirika la ndege la KLM,si nzuri kihivyo kama nilivyozani,airport ya dubai ina vyoo vingi vya kisasa vya electronics,mfano ukimaliza haja zako huitaji kuflash vina flash automatic,pia ni visafi muda wote na vina nukia marashi muda wote. Pia kuna mwanga mkali sana na kila kitu kipo kwenye mpangilio mzuri..ukimaliza haja zako mahali pakunawa kuna maji aina mbili,ya moto na baridi muda wote..haijalishi ni usiku au mchana..pia imesheeni lift nying kila kona..
Usafiri wa dubai,niwakisasa sana yaani
taxi zao ni nzuri sana,na unachajiwa gharama kupitia kisoma mita..huna haja ya kubageni bei
na dereva..wala huna wasi wasi kama ni mgeni utozwe pesa zaidi,maana kuna mita ya kusoma bei na umbali kwa dashbodi ya kila taxi ktk mji wa dubai,
metro train, ni usafiri wa haraka sana na wakisasa sana ,ni tren za umeme ziendazo kwa kasi zaidi..utaratibu wahizi tren zimetapaakaa kila kona ya mji kuna vituo vya metro,unaweza tumia RT card au pesa taslimu kwa station ya metro,na nisafi sana ndani,na nigharama na fuu sana bus town trip, usafiri huu ni wakisasa sana..mabasi yao ni mazuri kuna ya aina 3 ya ghorofa,marefu saana,nay a kawaida ,ila yote yana ac muda wote,na hakuna kukanyagana wala kubabanana..pia kuyatumia unaitaji uwe na card,kila kituo kina mashine yakununua card.
Itaendelea kesho.....
0 comments:
Post a Comment