Kuanzia mwaka 2010, asasi isiyo ya kiserikali ya Interconnectedness Foundation ya Uholanzi imekuwa ikiendesha siku maalum ya kuwaleta watu popote duniani pamoja- siku hiyo maalum ni Novemba 11 ya kila mwaka, lengo ni kupata wasaa wa kutafakari mazuri ya kuwepo duniani kwa kuhimiza furaha na amani.
Siku hiyo imepata umaarufu katika mabara yote, na mabalozi mbalimbali wa Foundation hiyo wamekuwa wakiendesha matukio mbalimbali kama vile burudani za muziki,maonyesho au makongamano yenye lengo la kuhimiza utunzaji wa mazingira, umakini katika masuala ya kiroho, na haki kwa watu wote.
Leo 11-11-2011 tunasherehekea tena siku hiyo maarufu kama Interconnectedness Day.
Je, siku hii kibongo bongo vipi ?.
Kwa maelezo zaidi na kama wataka kuwa balozi wa Interconnectedness Foundation, BOFYA HAPA
0 comments:
Post a Comment