Yule mchungaji Xola Skosana wa Cape Town, Sauzi, mbali na kutumia mahubiri ya Yesu ana Ukimwi, kuhamasisha watu kuwa makini na Ukimwi, amewahi kufanya vituko kadhaa hapa Sauzi. Ikumbukwe pia alikanusha kumdharirisha Yesu, akidai lengo lake la kusema Yesu ana ukimwi ilikuwa ni kutoa mfano.
Mwezi April mwaka huu alitembea umbali wa Kilomita karibu 14 akiwa amebeba msalaba akidai kuwa kitongoji anachoishi na vitongoji vingi vya Sauzi ni kama Ahera, kwani huduma za kijamii ni mbaya, ubinafsishaji wa huduma za maji,umeme na elimu, na kuondolewa kwa wakulima katika mashamba yao kupisha miradi ya maendeleo.
( Habari na: abahlali.org , christianpost.com Picha na : sowetanlive.co.za)
0 comments:
Post a Comment