MAMBO KAMA YALIVYO NJE YA TANZANIA

Friday, 21 October 2011

WANAUME WASIOTOA MATUNZO KWA WATOTO WAO WAKAMATWA SAUZI

10:12 By Mindset


Serikali hapa Afrika Kusini ipo katika kampeni ya kukamata wanaume wote ambao majina yao yaliorodheshwa kuwa wanahitajika kulipa fedha za matunzo za kila mwezi za watoto wao ila wamekaidi agizo hilo.

Hii inafuatia utaratibu uliopo nchini hapa kwamba kama mwanaume ana mtoto wake na hakai na mlezi mwenzake basi inabidi ampatie fedha za matunzo mtoto wake kupitia serikali, lakini kuna baadhi ya wanaume wamekaidi agizo hilo na ndio wanaosakwa.

Tayari wanaume 58 wameshakamatwa toka kampeni maalum iitwayo Isondlo, idadi kamiri ya wanaume wanaotafutwa katika kampeni hiyo ni 819. Kati ya hao 58, wanaume 7 walijisalimisha wenyewe.

Kampeni hiyo pia inakusudia kuwatafuta akina mama ambao wameacha kwa muda mrefu kupokea fedha za matunzo ya watoto wao toka serikalini. Kampeni hii inasimamiwa na wizara ya sheria na maendeleo ya katiba ya hapa Afrika kusini.

Habari zaidi Bofya hapa

Comment yetu: Hivi hii kibongo bongo itakuwaje kama wakianza kusakwa...?

0 comments: