MAMBO KAMA YALIVYO NJE YA TANZANIA

Friday, 21 October 2011

STEVE JOBS ALIPUUZIA MATIBABU YA KANSA- WASIFU WA STEVE JOBS WAELEZA

10:53 By Mindset


Muasisi wa kampuni ya Apple, Steve Jobs anadaiwa kukataa kwa makusudi operesheni ambayo ingeweza kuokoa maisha yake, na badala yake akachagua kutibu kansa kwa vyakula (diet), kwa maombi na aina nyingine za matibabu  isipokuwa upasuaji.
Tena kuna wakati aliwadanganya watu kuwa eti ameshapona kansa wakati ukweli ulikuwa alikuwa akiendelea na matibabu kisirisiri.
Steve Jobs anatambulika kuwa alikuwa msiri sana wa masuala yake binafsi hadi alipoamua kumtumia Walter Isaacson kuandika wasifu wake ambapo anaeleza mambo mengi kwa uwazi kuhusu maisha yake.
Steve Jobs atakumbukwa kwa mengi ikiwa pamoja na uasisi wake wa Macintosh computer, iPod, iPhone na iPad.
Habari hii ni kwa mujibu wa yahoonews, ikiripoti mahojiano ya muandika wasifu wa Steve Jobs - Isaacson,  kama alivyohojiwa na CBS. 
Fuatilia habari hii zaidi BOFYA HAPA
COMMENT yetu: Hivi inakuaje wajameni mtu jiniazi kama huyu kupuuzia jambo muhimu kama hili ?

0 comments: