MAMBO KAMA YALIVYO NJE YA TANZANIA

Monday, 24 October 2011

TAMADUNI YA KUZIKA MAPACHA PAMOJA HATA KAMA SI WOTE MAREHEMU-SAUZI

10:26 By Mindset


Hapa Sauzi, hususani kwa watu wa kabila la Xhosa, wana tamaduni ya kustaajabisha kuhusu mapacha.

Kama pacha mmoja atakufa, basi mwenzake hata atazikwa nae. Kama pacha mwingine hajafa, ni lazima aingie kwanza kaburini akae kidogo kama dakika kadhaa kisha atoke. Halafu ndipo mwili wa pacha marehemu utaingizwa kaburini na kufukiwa.
Na cha kuongeza ni kuwa kaburi la pacha huandaliwa kiasi kwamba zinakuwepo sehemu mbili za kuweka miili ya mapacha.


Na kwa upande mwingine wa maisha ni kuwa kama pacha anataka kuogelea baharini inampasa atupe sarafu ya madini ya silver vinginevyo atazama baharini.

0 comments: