Vipengele kadhaa ndani ya google plus |
Hivi ndivyo inavyoonekana ukiwa kwa akaunti yako ya google plus |
Kama bado haujajiunga na mtandao huu wa kijamii wa mawasiliano basi habari ndio hii.
Google imezindua rasmi mtandao huo unaoenda kwa jina la Google Plus, ambao ulianza kuwa wazi rasmi kwa watu wote tarehe 20 Septemba 2011 ambao kwa mujibu wa wikipedia.com watu waliojiunga walifika milioni 40 kwa mwezi huu wa Oktoba.
Google Plus inawezesha mtumiaji kuchat kwa video, na hata kuwa na sehemu tofauti za kuweka status, mfano waweza kuweka status ambayo marafiki zako tuu wataona, halafu ukaweka status sehemu nyingine ambako watu wako maalum kama mabosi wako au walezi wako waone.
Kupata taarifa zaidi na kujiunga na mtandao huu .Bofya hapa
Kumbuka: Kwa sasa mtandao huu hauruhusu mtu mwenye umri chini ya miaka 18.
0 comments:
Post a Comment