MAMBO KAMA YALIVYO NJE YA TANZANIA

Tuesday, 18 October 2011

GHARAMA ZA MAISHA - MALAYSIA

13:08 By Mindset

Malaysia, ipo Asia ya Kusini kama unavyojionea kwa ramani na majirani zake
Taswira ya jiji la Kuala Lumpur - Mji mkuu wa Malaysia


Ifuatayo ni orodha ya gharama za maisha kwa wastani kama alivyotutumia mdau wetu aliyepo Malaysia:

Kodi ya chumba kwa mwezi ni dola za  kimarekani 100, ila tukizungumzia on average chumba cha kawaida tuu ni kati ya US $ 150 mpaka US $ 200. Hiyo ni bei ya chumba uswahilini. Fedha ya Malaysia inaitwa Ringits, ambapo $1 = 3 Ringits

Kwa usafiri wa 'daladala' kama mizunguko yako ya kawaida yaani nyumbani -ofisini au shuleni, basi waweza tumia kama US $ 10 kwa siku.

Upande wa misosi, utapata kazi kutafuta mama ntilie, ila restaurant na hotel ni nyingi. Kwa chakula cha kawaida mijini ni kuanzia US $ 2 na ushe, tuseme  kuanzia US $ 3.

Kuhusu mavazi na nguo ni gharama sana, ni kama mara nne ya bei unayoweza kupata bongo. Ila kiubora, zipo juu.

Hapa pia hakuna maduka madogo madogo ila utakuta supermarkets kibao. 

Gharama za masomo kwakweli zipo chini sana ukilinganisha na aina husika ya masomo katika nchi nyingine zilizoendelea.

Ajira kwa hapa Malaysia ni ngumu sana hasa ukiwa foreigner. Labda uwe umetoka nayo nchini kwako yaani labda umetumwa na shirika au kampuni imekuhamishia hapa. Ni ngumu sana kama mtu hauna elimu ya kutosha kutengeneza kipato halali hapa.

Ila wapo wasanii kibao na hata wauza madawa, bali kuna sheria kali sana mfano mtu akikamatwa na madawa ni kifo tuu.

N: B, Shukrani za pekee kwa mdau wetu aliyepo huko Malaysia masomoni.




















0 comments: