MAMBO KAMA YALIVYO NJE YA TANZANIA

Monday, 24 October 2011

MANCHESTER CITY ILIVYOIADABISHA MANCHESTER UNITED

11:05 By Mindset



Mabingwa wa Ligi kuu ya Uingereza, Manchester United walipata kipigo cha kihistoria siku ya Jumapili Oktoba 23,2011 kwa kulazwa mabao 6 kwa 1 tena uwanja wa nyumbani, Old Trafford.


Kabla ya kipigo hicho Manchester United imeshacheza mechi 37 bila kufungwa. Kipigo hicho cha mabao 6-1 ni cha pekee kwani mara ya mwisho wa Manchester kufungwa magoli mengi kiasi hicho katika Uwanja wake wa Old Traford ilikuwa mwaka 1955.


Mabao ya Manchester City yaliwekwa kimiani na Mario Balotelli na Edin Dzeko waliofunga magoli mawili kila mmoja, wengine ni Sergio Aguero, na David Silva.



0 comments: