1. Tambua chanjo unazohitajika kufanya kabla ya kuingia nchi husika. Mfano kama wataka kwenda Afrika Kusini basi ni lazima uwe umechanjwa chanjo ya Homa ya manjano.
2. Hakikisha una Passport isiyoisha na halali, na Visa husika ya kuingia nchi fulani. Kama nchi unayotembelea haikulizimu Visa kuingia ni vema.
3. Hakikisha unafahamu sarafu ya nchi unayoenda, na unajua kiwango cha mbadilishano wa fedha ulizonazo na fedha ya nchi husika. Hii ni muhimu ili kukuwezesha kuwa na kiwango sahihi cha fedha unachohitaji katika nchi ya kigeni.
4. Fanya 'Home work' ya kujua gharama za maisha za nchi unayoenda mfano bei za vyakula, maladhi na usafiri, na kama una mpango wa kufanya Shopping basi ujilidhishe na taarifa ya awali ili usije ukaishiwa kabla ya wakati ukiwa ugenini.
5. Tambua eneo husika utakalofikia, umbali na usafiri na gharama zake kabla haujasafiri usije ukarubuniwa na wajanja wa sehemu husika.
6. Kuwa makini na mizigo yako ufikapo sehemu husika, usiulize kila mtu kuhusu mahali au jambo fulani na chukua tahadhari zote za vibaka, na walaghai kama hao, wapo kibao hata nje ya Tanzania.
7. Check afya yako kabla haujasafiri na ikiwezekana chukua madawa ya tahadhari na kama waweza jua namna ya kupata matibabu na huduma za matibabu kama vile bima za afya n.k katika nchi husika. Kuumwa kupo na ni mbaya kama hukujiandaa na gharama au kuwa na akiba ya dawa za dharula.
8. Jifunze kuheshimu na kutambua tamaduni ngeni kwani mambo mengi unaweza kukutana nayo mageni nje ya Tanzania. Kuwa mtu mwepesi wa kujichanganya na watu na kupenda watu, ila kuwa makini sana na matapeli.
9. Jifunze walau kwa uchache lugha ya sehemu husika, hususani salamu, kusema samahani, au kuuliza mahali husika.
10. Usijionyeshe kuwa mgeni, ikiwezekana vaa kama wenyeji wa sehemu husika na fuata tamaduni ya sehemu husika ili uepuke kupata shida na wahalifu.
11. Fuata taratibu husika katika kupiga picha watu au maeneo husika, kuna wakati itakupasa uulize mwenyeji kama unaruhusiwa kupiga picha sehemu fulani.
0 comments:
Post a Comment