MAMBO KAMA YALIVYO NJE YA TANZANIA

Friday, 14 October 2011

BACKPACKER - KAMA UNAJALI KUBANA MATUMIZI UKIWA NJE YA BONGO

10:08 By Mindset

Hapa Mdau, nikiwa kwa HOLIDAY BACKPACKER, Cape Town
Hapa ni kwa nje ya Holiday Backpacker- Cape Town

Backpacker ni aina ya nyumba ya wageni maalum kwa wasafiri ambao wana mpango wa kubana matumizi ili uweze kuienjoy safari yako.


Malipo ya Backpackers ni nafuu kuliko hoteli za kawaida, na mara nyingi kuna option tofauti tofauti, mfano waweza kukodi chumba kizima peke yako au ukalala kwenye chumba maalum ambacho ni bweni  hicho utakuwa upo na wasafiri wengine.

Backpackers nyingi tofauti na hoteli, hazitoi huduma za chakula, isipokuwa nyingi huwa na sehemu ya jiko na friji pamoja na sehemu ya kula chakula - dining room.
Hivyo waweza nunua chakula chako nje - take away au ukaamua kujipikia hapo na ukahifadhi kwa friji.

Ila uwe makini na mali zako na vitu vingine kwani mahali popote palipo na wengi bwana, vibaka hawakawii kuharibu mazingira.

John., Sauzi.

0 comments: