Mpambano wa soka kati ya timu kongwe ya mjini Cairo ya Al Ahly na timu ya Al Masry ulibadilika baada ya kipenga cha mwisho na kuwa mpambano wa mashabiki wa timu hizo ambapo watu wapatao 74 waliuwa katika mapambano hayo.
Mechi ya soka kati ya Al Ahly na Al Masry ilifanyika siku ya Jumatano, Februari 1,2012 ambapo timu ya Al Masry iliifunga timu mwenyeji ya Al Ahly kwa mabao 3 kwa 1.
Wakati wa mpambano wa mashabiki wa timu hizo mbili, polisi wanadaiwa walikaa pembeni wakishuhudia mpambano huo, bila kuchukua tahadhari au kuzuia machafuko hayo. Wengi wa watu waliouwa ni kwa sababu kulikuwa na milango midogo ya kutokea uwanjani hapo ambapo milango hiyo ilikuwa ni kama mtego kwa yeyote aliyepita hapo alipata kipigo cha hali ya juu ikiwa pamoja na kuchomwa visu.
Vifo vya watu hao 74 vimeleta gumzo na maandamano mapya ya kisiasa nchini Misri wananchi wakitaka uongozi uliopo madarakani kuachia ngazi.
Tayari polisi wameshaua waandamanaji wawili na kujeruhi kadhaa.
Habari na picha kwa hisani ya huffingtonpost.com
0 comments:
Post a Comment