Picha hii ya mtoto aliyekwisha mwili kwa kukosa chakula, ilipigwa mwaka 1993 huko Sudan. Mtoto huyo alikuwa akielekea kufuatilia mgawo wa chakula katika kambi ya Umoja wa Mataifa iliyokuwepo umbali wa kilomita 1 toka mahali ilipopigwa picha.
Ukiangalia vizuri utaona jinsi ndogo huyo mkubwa anavyomsubiria kwa hamu mtoto huyo afe ili ale mzoga.
Mpiga picha wa picha hii- Kevin Carter alijiua miezi mitatu baada ya tukio hili ikisemekana na kutokana na msongo wa mawazo kwa hali mbaya ya maisha aliyoiona huko, na masikitiko binafsi kwani inadaiwa alitumia karibu dakika 20 kupiga picha hii.
Picha hii ilishinda tuzo ya picha bora za mwaka 1994 za Pulitzer.
1 comments:
inahuzunisha sana ujue.... watu wengine wanamwaga chakula wengine ndy hivyo eeeh Mungu tusaidie waja wako
Post a Comment