Mei 1, 2001 Ramon Stoppelenburg (kuzaliwa Desemba 20,1976) alianza safari ya kutembelea nchi kadhaa, safari iliyomchukua muda mrefu hadi Julai 26, 2003 akitembea nchi kadhaa kwa msaada wa wenyeji wake katika nchi alizotembelea.
Kuna sehemu hakulipa kabisa hata nauli ya ndege, wakati baadhi ya sehemu alipata hifadhi ya malazi na chakula tuu.
Aliweza kufanya safari yote hiyo, kupitia blogu yake ya letmestayforoneday.com ambapo ili kulipa fadhila ya wenyeji wake aliandika makala kadhaa kwa blogu yake kuelezea sehemu husika aliyokuwa amefikia.
Kwa sasa Ramon, anaishi Cambodia, ila anaendesha kampuni ya Kuwaleta watalii mlima kilimanjaro ambao yeye mwenyewe aliupanda mwaka 2008.
Nchi alizotembelea ni Netherlands, Belgium, France, England, Ireland, Scotland, Northern Ireland, Wales, Denmark, Norway, Sweden, Austria, South Africa, Spain, Australia na Canada.
Je, wewe wasemaje Ubunifu huu wa kupata safari za dezo..? Tuandikie comment.
Kuona blogu iliyompatia umaarufu BOFYA HAPA
0 comments:
Post a Comment