MAMBO KAMA YALIVYO NJE YA TANZANIA

Thursday, 13 October 2011

WASEMAVYO WADAU WETU KUHUSU MAISHA NJE YA BONGO

11:24 By Mindset


Huu ni mwanzo wa mfululizo wa Maelezo ya Wadau wetu kuhusu experience na mtazamo wao wa maisha nje ya Tanzania. Wewe pia unaweza shiriki  kwa kutuma maelezo yako kwa email: john.myungire@gmail.com
Kama una swali lolote pia kuhusu mambo ya nje ya Tanzania, basi tuandikie, nasi tutalifanyia kazi.

 Ester Japhet, aliwahi kuwa India kwa Miaka Minne, Masomoni, sasa yupo Bongo anasema:


"Kabla sijatoka TZ nilikuwa najua kuwa maisha ya nje ya bongo sio magumu unaweza kuishi bila kufanya kazi kama unavyojua wazungu wanatoa misada kwetu sasa baada ya kutoka nikajua kuwa hata nje ya bongo maisha yanatafutwa kwa nguvu zote, ndio maana nikasema nilipata kufunguka na hata nikitoka hapa TZ najua kuwa huko niendako lazima nitafute kwa nguvu. Wapo watu India hawana nyumba wanalala barabaran. Si ajabu ukiwa nje ya Tanzania mtu akikuambia nitumie $ 200 ukimwambia sina anajua kuwa umemnyima".

Abdulsabury. Kwa sasa yupo Ujerumani anasoma Masters Degree, huku akifanya kazi anasema:


"Kama mtu anataka elimu bora huku ni sehemu nzuri sana ya kupata elimu bora,but ukimaliza shule kama hukupata kazi ni bora kurudi home. Life ni tyt sana, tatizo ni pesa unapata but maisha huku ni too expensive. Huku soda ni euro 1 hivi chumba cha chini kabisa ni euro 190 to 200
Kama unafanya proffessional jobs unaweza ukatengeneza pesa,but kama unafanya kazi za kawaida 4get man life huku sio simple kama watu wanavyodhani. Sehemu zenye mazingira yalichoka kama baadhi ya sehemu za Dar ni kibao tu! "


Shukrani kwa wote wanaotuma maelezo ya experience zao nje ya Tanzania. Tutaziweka hewani zote.

0 comments: