MAMBO KAMA YALIVYO NJE YA TANZANIA

Thursday, 20 October 2011

SIMBA, TWIGA, CHUI WAJIVINJARI MTAANI- MAREKANI

12:49 By Mindset


Iliwahi kutokea Bongo kuwa wananchi walikuwa katika wasiwasi wa kuwa simba yupo mtaani na hofu ilitanda katika maeneo kadhaa ya jiji la Dar es salaam.

Hali hii sasa imeikumba Marekani, eneo la OHIO, si uzushi na ni halisi kama unavyojionea katika picha hapo juu tangazo likionyesha kuwa wananchi wawe makini kwani wanyama pori wakiwemo simba, chui, wamezagaa maeneo kadhaa karibu na jamii.

Wanyama pori wanaokadiriwa kufika 56 waliponyoka toka katika zizi lao baada ya 'mmiliki' wake aliyetambulika kwa jina la Terry Thompson (miaka 62) kuwaachia huru na kisha kujiua.

Kikosi maalum cha askari kilifanikiwa kuua wanyama 49 kati ya hao 56 na katika wanyama waliouawa 17 walikuwa simba na 18 ni chui.

Hii ni kwa mujibu wa CNN

0 comments: