MAMBO KAMA YALIVYO NJE YA TANZANIA

Wednesday, 12 October 2011

FACEBOOK INAKUSUMBUA ? HUDUMA HII MPYA NI BALAA.....

10:57 By Mindset


Hii toka South Africa, ambapo hapa kuna huduma ya kuchati inayoitwa Mixit.

Huduma hii inawezesha watu kuchat kama wanavyoweza kufanya kupitia facebook, yahoo messenger, skype, googletalk, n.k

Zaidi ya yote huduma hii ni nafuu sana na inatumika zaidi kwa njia ya simu. Inasemekana urahisi wa huduma hii ya kuchati ni mara kumi ya kutuma meseji kwa njia ya simu. Unachotakiwa ni kudownload kwa simu yako kisha unatumia. Unaweza pia kujiconnect na huduma nyingine za chat kama facebook, yahoomessenger.

Kampuni inayosambaza huduma hiyo (Mixit Lifestyle (Pty) Ltd haitozi gharama yoyote, ila makampuni ya simu hutoza kiasi kidooogo cha fedha kutuma meseji kupitia huduma hiyo ya Mixit.

Huduma hii ipo pia nchi jirani ya Kenya. Kwa mujibu wa wikipedia.com Mixit ina wateja takriban Milioni 27 na karibu wateja 40,000 wanajiunga kila siku, hii inaifanya kuwa social network kubwa zaidi barani Afrika.

Hii ikifika bongo, si balaa jamani ?
Sema chochote ! comment au tuandikie kwa john.myungire@gmail.com

0 comments: