MAMBO KAMA YALIVYO NJE YA TANZANIA

Wednesday, 19 October 2011

DAKTARI WA KITANZANIA ALA TUZO NJE YA BONGO

14:57 By Mindset


Dr. Julie Makani, ambaye anafanya kazi hospitali ya Muhimbili, Dar es salaam, amepata tuzo inayoitwa The Royal Society’s Pfizer Award  na aliipokea zawadi hiyo tarehe 18,11,2011 huko Uingereza.


Tuzo hiyo ambayo ni kitita cha paundi 60,000 kwa ajili ya kuendeleza utafiti ambao Dr. Makani na timu yake waliuanza kuhusu ugonjwa wa Anaemia na Sickle Cell huko Tanzania.


Katika tuzo hiyo pia kuna fedha za mshahara wake binafsi, pamoja na zawadi nyingine binafsi ya paundi 5000.


Tuzo hizo maalum kwa ajili ya tafiti za kibailojia zinatolewa kila mwaka na taasisi ya  Royal Society na kudhaminiwa na kampuni ya Pfizer Limited. 


Kwa maelezo zaidi ya jinsi ya kushiriki tuzo hizo BOFYA HAPA


Kwa niaba ya wadau wa nje ya bongo.com, tunasema hongera sana Dr. Makani. 

1 comments:

Magam said...

Huu ni mfano wa kuigwa, hongera sana Dr. Makani