Mganga wa jadi (sangoma) mmoja hapa Sauzi, amekuwa gumzo baada ya kuibua madai hadharani kuwa eti analidai TFF ya hapa SAUZI yaani (SAFA) takribani Randi 90,000 sawa na Shilingi 20,070,000 za kitanzania.
Mganga huyo anayejulikana kwa jina la S'bonelo Madela amedai kuwa aliiwezesha timu ya taifa ya Sauzi - Bafana bafana kushinda mechi yake ya kombe la dunia 2010 dhidi ya Ufaransa na kwamba SAFA haikukamilisha kitita walichoahidiana.
Sangoma huyo anaendelea kudai kuwa kama SAFA haitomlipa basi Bafana bafana itaendelea kufanya vibaya katika mechi zake zote, na ndio maana Bafana bafana haijaweza kupita katika mchujo wa kwenda kwenye fainali za mataifa ya Afrika mechi iliyofanyika jumamosi iliyopita.
Makamu wa raisi wa SAFA aitwaye Mwelo Nonkonyane amekaririwa na gazeti la The Daily Sun la hapa Sauzi, akiriri kuwa SAFA ilitumia huduma za sangoma huyo ila akadai walichampa 'chake' mapema. Hata hivyo katika libeneke la kickoff, makamu huyo wa raisi wa SAFA amekanusha kutoa matamko ya kuwa SAFA ilitumia huduma za huyo sangoma.
Habari ndio hiyo..!!!
Maelezo- Mdau, toka Sauzi- na magazeti ya ( Mail and Guardian Online na Kick off).
Kama wataka soma zaidi habari hii BOFYA HAPABOFYA HAPA
0 comments:
Post a Comment