Napenda kushare taarifa ya aina ya biashara ambayo kwa kiasi kikubwa bongo inaonekana kama ni biashara ndogo au ya watu wa hali ya chini ila hapa Sauzi, biashara hii inafanya na makampuni makubwa yanaondesha supermarket.
Ni biashara ya kuuza firigisi (gizzards), miguu ya kuku (chicken legs) na hata mikia ya kuku (chicken tails).
Walichoweza kufanya wenzetu ni kurasimisha hii biashara kwa kuboresha ubora wa mapishi na usafi na kipimo cha namna ya kununua.
Supermarkets nyingi waweza nunua viungo hivyo vya kuku vikiwa vimepikwa vyema , ila kama hautaki vilivyopikwa, waweza pia nunua visivyopikwa na ukaenda kupika.
Hii si tuu kwa nyama ya kuku, ni kwa aina zote za wanyama wanaoliwa, hata makongoro waweza yapata yakiwa yamewekwa vyema kwa wewe kununua.
Naamini hata sisi bongo twaweza hili, mfano mtu waweza fungua kibanda chako safi cha kisasa, ukaenda kwa masokoni wanapochinja kuku, na kununua hivyo viungo vya kuku, na ukavikaanga safi, na kuviandaa kwa rosti nzuri au viungo vya mboga(spices) vyema na ikawa biashara ya kuendesha maisha.
Yes, hakitupwi kitu, nyama ni nyama !
Kama wahitaji mjadala zaidi jinsi ya kufanya biashara hii hapo bongo, wasiliana nasi kwa email: john.myungire@gmail.com
John, Sauzi.
0 comments:
Post a Comment