MAMBO KAMA YALIVYO NJE YA TANZANIA

Thursday, 31 May 2012

BLOGU HII IMESAMISHWA KWA MUDA

Kutokana na Sababu za kiutendaji , Tumeamua Kusimamisha Kuchapisha Makala za blogu hii mpaka hapo tutakapowataarifu tena.

Tunasikitika kwa Usumbufu Utakaojitokeza.

Kwa Sasa Tafadhali tembelea Johnie Blog


Monday, 16 April 2012

JACOB ZUMA KUOA TENA WIKIEND IJAYO

Picha na wikipedia

Raisi wa jamhuri ya Afrika ya Kusini, anatarajiwa kuoa tena wikiend ijayo, mara hii atakuwa anafikisha mke wa NNE.

Kwa mujibu wa habari nilizoshuhudia kwa vituo vya television vya hapa Sauzi, pia kujionea katika magazeti ya jana Jumapili, inadaiwa raisi Jacob Zuma atafunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu bi Bongi Ngema, ambaye kwa mujibu wa www.iol.co.za raisi Zuma na bi Bongi Ngema tayari wana mtoto wa miaka minne.

Kwa mujibu wa www.iol.co.za Msemaji wa raisi Mac Maharaj amewaondoa wananchi hofu kuwa raisi atatumia hela zake binafsi na hakuna hela ya mlipa kodi itakayotumika katika kufanikisha sherehe hiyo ya harusi ambayo itakuwa ni shughuli binafsi.

Thursday, 12 April 2012

GHANA WAJIPANGA KUCHUKUA KOMBE LA AFRIKA MWAKANI

Aliyekuwa nahodha wa timu ya taifa ya Ghana ,  Kwesi Appiah ameteuliwa kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya Ghana -Black Stars.

Kwa mujibu wa ghanaweb.com , Appiah amepewa ulaji wa mkataba wa miaka miwili na ana kibarua kizito cha kuhakikisha malengo ya taifa hilo katika soka yanafikiwa, malengo hayo ni kuhakikisha kuwa katika fainali ijayo ya dunia Ghana inafika Nusu fainali na katika fainali za kombe la mataifa ya Afrika, taifa hilo linabeba kombe hilo.

Haya kazi ndiyo hiyo, wenzetu wa Ghana wameweka malengo.  
Toa maoni yako, kwetu sisi wabongo, tuna malengo yapi na tumejipangaje kufikia malengo hayo kwa kombe la dunia na kombe la mataifa ya Afrika ?

Thursday, 15 March 2012

NJAA MAREKANI

Kwa wale wabongo wenzangu wanaodhani kuwa huko ughaibuni maisha ni marahisi sana, jionee mwenyewe website hii inayoeleza maisha yalivyo magumu hata huko Marekani.

Website hii ni sehemu ya mpango wa kitaifa huko Marekani kusaidia wale wanaokosa msosi. Inadaiwa kati ya watu 6 Marekani, basi 1 ana tatizo la kutokuwa na uhakika wa msosi.

Una Maoni ?

Tembelea website hii kwa kubofya HAPA

Tuesday, 6 March 2012

SAUZI; MALIPO YA DALADALA KWA 'VOCHA'


TAP- I -FARE ni huduma inayomuwezesha abiria kulipia usafiri wa daladala kwa kutumia kadi maalum badala ya kutumia fedha taslimu.

Huduma hii imeanza rasmi huko Cape Town, Afrika Kusini na kwa sasa ipo katika kipindi cha majaribio.

Huduma hii inaendeshwa na kampuni ya Integrated Fare Collection Servives (Pty)Ltd (IFCS).
Maelezo kwa hisani ya http://tapifare.com/

Monday, 5 March 2012

MBWA NAO WANAANGALIA VIPINDI VYAO MAALUM VYA TV

Huduma maalum ya vipindi vya Television (runinga) kwa ajili ya mbwa ili wanapobaki peke yao majumbani waweze kutulia imeanzishwa huko Marekani.

Wamiliki wa mbwa wenye kuhitaji huduma hii wanalazimika kulipa $4.99 takribani Tshs.7985 kwa mwezi.

Swali: Je, huduma hii inaweza kuleta faida kwa kampuni husika inayoandaa program hizo za TV kwa ajili ya mbwa ?

Picha na habari kwa hisani ya www.businessweek.com

Friday, 2 March 2012

MLIMANI CITY INGEKUWA HIVI , INGEKUWAJE ?

Baadhi ya Supermarket huko Marekani zimeweka huduma ya vigali vidogo kama unavyoona pichani hapo juu ambapo mteja anaweza kuendesha akizunguka huku na kule humo ndani ya supermarket ili kujionea kile anachohitaji kununua.
Je, vigali hivi vingekuwa vinatumika Bongo sehemu kama Mlimani City, hali ingekuwaje ? Toa Maoni Yako.

Thursday, 1 March 2012

GOOGLE NA SERA MPYA: ZITAMBUE ZINAVYOATHIRI UHURU WAKO


Kuanzia leo Tarehe 1, Machi 2012 Google imeanza kutumia sera yake mpya inayoruhusu kufuatilia taarifa zako kama ulivyoziorozesha wakati wa kujiandikisha katika huduma zake, pamoja na zile unazobadilishana na watu mbalimbali.

Lengo kuu la Google kufanya hivyo ni ili kuweza kukuletea Mapendekezo Yanayokulenga moja kwa moja.

Mfano; kama umezoea kuandika email (barua pepe) kwa John na kisha ukaicopy kwa Mussa, basi kila utakapoandika email google yaweza kukupa pendekezo la kujumuisha na email ya Mussa.
Mfano mwingine ni kama unatafuta wimbo fulani kwa youtube Google inaweza pendekeza wimbo mwingine kuendana na historia inavyojionyesha kuwa wewe unapendelea nyimbo za namna gani.

Hii pia inasaidia Google kukuletea matangazo yanayokuhusu moja kwa moja. Mfano kama kipindi hiki umekuwa sana ukifuatilia habari za kazi basi usishangae ukiwa unasearch nyimbo kwa youtube Google ikakuletea tangazo la kazi.

Ni hayo tuu kwa leo, kujisomea zaidi kuhusu Sera hii na jinsi ya kujihadhari BOFYA HAPA